MASOMO
1.Mwa.
12: 1-4a
2.2Tim.
1: 8b-10
3.Mt
17:1-9
TAFAKARI: KUITWA KWA ABRAHAMU NA MUNGU KUWE MFANO WA
KUIGWA NA SISI TULIO WAFUASI WA KRISTU.
Tukiwa
tunaadhimisha dominika ya 2 ya Kipindi cha Kwaresma tunaalikwa kutafakari juu
ya masomo yetu Jumapili ya leo. Tukianza na somo la kwanza tunamwona Baba yetu
wa Imani, Abrahamu anaitwa na Mungu. Miaka takribani 1850 Kabla ya Kristu
ilikuwa ni mpango wa Mungu kuleta mabadiriko katika Historia ya mwanadamu.
Mungu alimchagua Abrahamu ambaye amekuwa Baba yetu kiimani ambapo kupitia kwake
wokovu ulikuja duniani.
Kipindi Abrahamu alichoishi kilikuwa
ni kipindi ambapo nchi ya Mesopotamia ilikuwa nchi ambayo ilikuwa imeendelea
kiuchumi, kitechnolojia, Kielimu na Pia ilikuwa ni nchi iliyojaliwa rutuba ya
kustawisha mazao mbalimbali. Abrahamu mbali ya kukaa katika nchi iliyokuwa na
maendeleo ya namna hiyo Abrahamu anaambiwa na Mungu kuhama nchi ile na kwenda
nchi asiyoijua.Abrahamu baada ya Kusikia sauti ya Mungu anachukua uamuzi wa
Kuhama nchi yake na kwenda nchi asiyoijua bila ya kusita. Kwa macho na akili ya Kibinadamu siyo rahisi
na si jambo jepesi mtu kuacha nyumba
yake, mali, na mfumo mzuri wa maisha na kwenda nchi isiyojulikana. Hapa
twajifunza suala juu ya Imani, yaani kusadiki hata tusiyoona. Mungu anayetuita
ndiye anayetuongoza na kutuonyesha mahala pa kwenda. Mungu atuitapo huwa
hatuonyeshi njia mojakwa moja, Silaha ya Imani, Matumaini na Sala ni nyenzo
Muhimu katika kutambua njia na kwenda ile nchi Mungu anapotuita kama Abrahamu
alivyoitwa.
Katika kutambua mwito wa Abrahamu
kuitwa kufanya kazi ya Mungu, tunajifunza somo la maisha ya kujitoa na pia
maisha ya sadaka kwa wengine. Tunaona katika somo la pili( 2Tim1:8b-10) Kipindi
Timothi anahubiri Injili ya Kristo kule Ephesus mambo yalikuwa siyo salama na
wale wote waliionyesha upinzani katika
Serikali ya Efesus hasa wahubiri Injili ya Kristu waliwekwa Kitanzini, hali
hiyohiyo ndo Timoth anakumbana nayo kule Efeso. Mtume Paul anaandika barua yake
ya kitume kule Efeso akiwafariji na kuwaambia kuwa “njia ya kumfuata Kristu
changamoto hazikwepeki” Maisha ya ufuasi wa Kristu yanamadai yake ambapo pia na
changamoto tunakabiliana nazo. Katika mazingira yetu tunaona sisi wakristu
tunakumbana na changamoto ambazo zinakabili kanisa letu hasa hapa Tanzania kama
vile Kuchoma makanisa moto nk.
Kutoka somo la Injili ( Mt 17:1-9)
tunaambiwa kuwa Yesu juu mlimani akiwa na wanafunzi wake alitimiza mapenzi ya
Baba yake na kuonyesha kuwa yeye ndiye alikuwa ukamilisho wa yote yaliyofanywa
na watangulizi wake, Musa na Manabii. Hapa tunaona Yesu akiwa na wanafunzi
wake, Yohane, Peter, na James. Pia Yesu anaonekana kuwa na Musa, na Eliya. Yesu
anageuka sura na kungaa kama jua. Swali la kujiuliza ni kuwa kwa nini Yesu
anaonekana akiwa na Musa na Eliya? Hii ina maana kuwa Yesu amekuja kukamilisha
Torati ( Musa) na Manabii( Eliya) Ni kwa msingi huo tunasema kuwa Kristu ndiye
ufunuo wa mwisho wa Sheria( Musa) na Manabii( Eliya). Kubadilika sura na kuwa mweupe ni ishara ya
uwepo wa Mungu katika utu wa Kristu. Wingu jeupe lilowafunika ni Ishara ya
uwepo wa Mungu. Tukumbuke katika kitabu cha Kutoka i.e, Kut 13:21, ilikuwa
ishara ya Mungu kuwa alikuwa na watu wake. Musa alipopokea Sheria kutoka kwa
Mungu pia kulikuwepo Wingu jeupe ambapo pia ilikuwa ni ishara ya kuwepo kwa
Mungu Kut 24:16-18.
Kristu anapobadilika sura
anatufundisha kuwa tuwe watu wa Mwanga na pia tuwe Mwanga kwa wengine( Matendo
mazuri kwa wengine) na tusiwe watu wa giza. Kristu anangaa kama jua, kwa msingi
huu ni kuwa yeye ni Jua la haki.
Katika Injili ya Mt. Lk9:32
tunaambiwa kuwa wakati yesu anabadilika
sura kule mlimani alikuta wanafunzi wake wamelala( Peter, John na James). Ni
mara ngapi tunakosa kuuona utukufu wa Mungu kwa sababu tunakuwa tumelala kiroho
japo kimwili tu wazima. Kuna vitu vingi ambavyo vyaweza kutufanya kulala
Kiroho, navyo ni maisha yasiyo na mwelekeo wa Kumtafuta Mungu Mungu, Maisha au
njia za mkato. Anasa zaweza pia kutufanya tulale kiimani na hivyo kuusahau ule
utukufu wa Kristu.
0 Response to "MAHUBIRI JUMAPILI YA 2 KWARESMA MWAKA A"
Chapisha Maoni