HISTORIA FUPI YA IBADA
YA ROZARI.
UTANGULIZI
Katika Kalenda ya
Kanisa Katoliki, huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi ni miezi ambayo imewekwa
kwa ajili ya Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo hiyo miezi huwa inasaliwa
rozari. Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa nini ifanyike miezi hiyo? Yafuatayo
ni majibu, mwezi wa tano umewekwa kwa heshima ya Bikira Maria kutokana na nini
kilitokea katika historia hapo nyuma. Mnamo Karne ya 16 mwezi watano kwa miaka
yote ulikuwa ni mwezi ambao sikukuu nyingi za kiserikali ndo zilikuwa
zikifanyika. Kanisa kwa kutambua hilo nalo likahidhinisha pia mwezi wa tano uwe
ni mwezi wa Rozari, na kwa makusudi zaidi Kanisa lililenga kuwa sherehe hizo
ziendane na taratibu za wakristu, ni kwa msingi huo sherehe hizo ziliendana na
mwezi wa rozari na kutokea hapo ikahidhinishwa kuwa mwezi wa tano wa mwaka ni mwezi
wa Bikira Maria. Pia mwezi wa kumi (October) pia ni mwezi wa Bikira Maria na
pia ni mwezi wa Kusali Rozari kutokana na historia ya hapo nyuma pia, na
ilikuwa kwamba baada ya ushindi wakristo walioupata katika vita baina yao na
yule aliyeitwa Lepanto mnamo 7 October, 1571, Papa wa wakati ule Papa Pius V
aliufanya huo ushindi kuwa ulitokana na maombezi ya Bikira Maria, na alisema
kuwa rozari ni silaha kubwa hata kuliko silaha kubwa za kivita. Ni Kwa msingi
huu tunaona kuanzia hapo mwezi wa kumi ukawa mwezi uliotengwa na Mama Kanisa
kwa Bikira Maria, na pia ukaitwa mwezi wa Rozari.
Historia
yenyewe
Ni kwamba sala ya
Rozari inasemekana kuanzishwa na Mt. Dominico aliyezaliwa mnamo mwaka 1170 na
kufariki mwaka 1221 na hiyo sala Mt. Dominico aliipata kwa njia ya ufunuo
ambapo Bikira Maria alimtokea na kumwamuru awe anasali rozari. Bikira Maria
alimwamuru mtakatifu Dominico kusali rozari kwa kipindi hicho iwe kama silaha
yake ili kupambana na uzushi uliokuwa umeibuka ukipingana na mafundisho ya
Kanisa, na huo uzushi uliitwa ‘ Albigensia’ hili ni kundi lilokuwa na imani
kuwa Duniani kuna nguvu nguvu mbili zenye uwiano sawa lakini hupingana na
kupigana moja baada ya nyingine, nazo nguvu hizo ni Mungu na Shetani. Hivyo
hawa waliamini kabisa kuwa Mungu na Shetani wana nguvu sawa ( Dualistic )
waliamini pia kuwa dunia hii imejaa uovu kwa kuwa iliumbwa na mwovu. Ni kwa
msingi huu Kanisa liliamua kupambana na hawa wazushi ambao pia walionekana
kupotosha mafundisho ya Kanisa. Ndipo tunaona Bikira Maria anamtokea Mtakatifu
Dominico na kumwambia asali rozari ili kupambana na mafundisho hayo ya kizushi.
Ni Papa Pio V ambaye mnamo mwaka 1569 alihidhinisha rasmi kusali rozari kwa
kanisa nzima na kuhidhinisha rozari iwe jinsi tunavyoiona sasa. Katika zile
zama za kati, watawa wamonaki walizoea kusali zaburi 150, na kwa upande wa
waumini walei ambao kwa kipindi hicho hawakujua kusoma zaburi iliwabidi wasali
sala ya Baba yetu mara 150 baadala ya zaburi 150 na hizo baba yetu walizisali
kwa kuhesabu punje 150 zilizokuwa zimefungwa kwenye kamba ndefu ambayo kwa
lugha ya kitaalamu iliitwa “ Corona” au kwa Kiingereza “ Crown”
kadiri ibada kwa Bikira Maria ilivyoendelea kushamiri mnamo Karne ya 12, sala
kwa Bikira Maria ilianzishwa na hivyo kuanza kusali salamu maria 150 baadala ya
baba yetu 150.
Salamu Maria 150 hapo
baadaye zilikuja kugawanywa katika makundi/ mafungu na Mtawa mdominica
aliyeitwa Henry Kalkar ( 1328-1408), ambapo kila tendo la rozari lilikuwa na
mafungu 50 ya salamu Maria ambapo pia kila fungu liligusia maisha ya Bikira
Maria na Yesu katika historia ya wokovu wetu. Zaidi ya hapo, mtawa mwingine wa
mdominican aliyeitwa Alanus de Rupe aliendelea kugawanya hiyo historia ya
matendo ya wokovu wetu katika matendo ya furaha,uchungu, na utukufu kama tunavyoyaona sasa. (NB Matendo
ya mwanga hayo ni ya majuzi siyo ya wakati ule). Na nikuanzia hapo Bikira Maria
amepewa nafasi kubwa katika shirika la watawa wa Dominican. Hivyo utamaduni wa
kusali rozari umeendelea karne hata karne, mfano Papa Leo XIII (1878-1903) aliweka
msisitizo mkubwa juu ya ibada ya rozari kwa Bikira Maria. Kuanzia September 1, 1883
Baba Mtakatifu Leo XIII aliandika jumla ya barua za kichungaji 11 zote zikiwa zinaweka
mkazo juu ya rozari. Hivyo rozari ni sala inayotokana na maandiko matakatifu( Biblia).
Mafumbo ya rozari yote yanapatikana katika agano jipya ambapo ndo tunaona matendo
ya Bikira Maria na Yesu Kristo katika wokovu wetu.
tunakumbushwa uchungu
aliopata Bikira Maria Katika maisha yake hasa ule utabiri wa Simeoni kwa Bikira
Maria juu ya mateso na kifo cha mwanae Yesu, Matendo saba ya furaha kwa Maria
ambapo yaananza na kupashwa habari kwa Bikira Maria na Malaika wa Bwana,
kupalizwa mbinguni, na matendo ya huruma ya Bikira Maria kwa wale ambao
wanaendelea kuteseka hapa duniani.
Asante kwa kunipa mwanga
JibuFutaNashukuru sana maana nlikuwa nkijiuliza sana kuhusu chimbuko la rozari takatifu
JibuFutaNimeelewa
JibuFutaAsante kwa kunijuza
JibuFutaAhsante kwa mafundisho
JibuFutaAhsante kwa mafundisho mazuri
JibuFutaNashukuru sana kwa hii historia. Mama Maria Utuombee.
JibuFutaAsante mama Bikira Maria utuombee.
JibuFutaI get you
JibuFutaAhsante kwa Mwongozo wetu
JibuFutaAsante na mbarikiwe
JibuFutaAhsante nyote pia kwa kusoma chapisho langu juu ya Rozari na Historia yake.
JibuFutalakini mbona kwenye biblia hakujaagizwa tusali rozari!?
JibuFutaSoma Matendo yote ya Rozari na hapo utaelewa kuwa hakuna ambacho tunakisali katika Rozari kipo nje ya Biblia. Hivyo kwa kusali Rozari pia ni kusoma biblia. Waweza sema kwenye Biblia hakuna hilo andiko ila Matendo ya Rozari yote kiini chake ni Biblia. Hivyo naweza hitimisha kuwa asili ya Rozari ni Biblia.
JibuFuta