MAHUBIRI YA
JUMAPILI YA 1 YA MAJILIO MWAKA A
MASOMO
1.Isa.2:1-5
2.Rum.13:11-14
3.Mt. 24:
37-44
TAFAKARI:
TUNAALIKWA KUJIWEKA TAYARI MDA WOTE ILI
KUMPOKEA KRISTO MASIHA MAISHANI MWETU DAIMA
Katika
Masomo ya leo, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kipindi kizima cha mwaka C wa
Kanisa ambao umemalizika na tumeanza kipindi kingine cha Mwaka wa Kanisa, yaani
mwaka A wa Kanisa ambao huanza kwa kipindi cha Majilio( Advent) kama miaka yote
tufanyavyo. Kipindi hiki cha Advent, ambacho asili ya neno Advent linatokana na
neno la Kilatini, yaani Adventus, maana yake kuja au “ ujio” Wakati wa Kipindi
cha Majilio kabla ya kuwepo Pasaka, kipindi hiki kilikuwa kinajulikana kama
kipindi cha kufunga( fasting) na kujinyima( abstinence) kwa ajili ya wahitaji
na ndiyo maana Padre au watumishi wa altare huvaa mavazi ya rangi ya zambarau
kama vile kwenye kipindi cha Kwaresma.
Kwa mantiki
hii ni kwamba kipindi hiki cha majilio kinatualika kujiandaa kwa ujio wa
Mwokozi wetu Yesu Kristu. Lakini yatupasa tujiulize kuwa ujio huu maana yake
nini?
Kwa
kutafakari juu ya hilo tunaweza kuelezea juu ya ujio wa Yesu Kristu kuwa ni wa
aina tatu. Ya kwanza ni kuzaliwa kwake, yaani umwilisho wake uliotabiriwa na
manabii( Incarnation), nafsi ya pili ya utatu mtakatifu, ya pili ni ni ujio wa
Kristu ambao huwa tunausibiri hata ukamilifu wa dahali. Katika kanuni ya imani
yetu hili limejielezea. Katika ule ujio watatu wa Yesu Kristu ni pale
tunapomsubilia yesu mfufuka ambaye yupo miongoni mwetu, huu ujio wa tatu
hauongelei Yesu aliyekufa na kuhaidi kuja au yesu atakaye kuja ( The await for
Jesus coming is not ascribed only in past or future, but it is also already in the
present). Ujio huo wa tatu wa Kristu kati yetu tunauona na tunaupata kupitia
huduma za kanisa kama vile Sakramenti na Neno la Mungu, hivyo ujio wa Kristu daima unakuwa kati yetu na
siyo hadi kipindi cha majilio.
Kutokana na
Mwanadamu kutokuwa mkamilifu, na kuanguka dhambini Mungu aliweka sheria kupitia
Sheria na Manabii kuweza kumkumbusha mwanadamu wajibu wake lakini hilo
halikutosha, hivyo Mungu aliamua kumtuma mwanae wa pekee kwa ajili ya wokovu wa
mwanadamu nah ii inadhihirishwa na Mtakatifu paul anaposema “ wakati ulipotimia
Mungu alimtuma mwanae duniani (Gal4:4)
Kuja Kwa
Kristo Yesu duniani na kujimwilisha kwake kulilenga kutangaza habari njema kwa watu wote wa kila
lika kama nabii isaya asemavyo “ Roho wa Bwana yu juu yangu, amenipaka
mafuta, amenituma kutangaza habari njema
kwa maskini, wafungwa, kufungua vipofu, na kwa walioonewa Na kutangaza mwaka wa Bwana.”( Cf.Lk4:18-19).
Ujio wa Kristu kwa mara ya pili unatualika sote tuwe tayari kwa kuwa hatujui
siku wala saa.
Kristu kwa
kuja kufanya vipofu waone, alikuja kuleta mwanga ambao ungelifungua macho na
moyo wa kila mmoja wetu, kuja kwake Kristu kwa maisha yetu kumefungua vipi
mioyo yetu kwa sasa na mazingira yetu tunayoishi hasa mazingira ya ushirikina, uchawi, utandawazi, technolojia,
(japo hatuhalalishi kuwa teknolojia ni mbaya ila matumizi yake mabaya kupita
kiasi ndiyo tatizo) ni wangapi wamefungwa macho yao na haya mambo kiasi cha kumsahau
Mungu, je sisi tuliofunguliwa macho tunawafungua pia ambao bado hawajafunguliwa
macho? Katika somo la Pili, Rum. 13:1-14
Mtakatifu Paul anatwambia juu ya kuvaa silaha za nuru, akimaanisha kuwa sisi ni
wana wabatizwa katika Kristu, hivyo inatupasa tuweke mioyo yetu tayari kwa
ajili ya Kristu. Kuna Mhubiri mmoja maarufu alisema haya “Tujitwalie siraha za
mwanga. Biblia ni siraha ya mwanga. Sala ni siraha ya mwanga. Jambo la msingi
ni kutumia siraha hizo. Breki kama hauzitumii utajikuta kwenye kichaka, kwenye
mtaro wa barabara.
Tusilale kwenye ulafi.
Ulafi ni uroho. Upapiaji chakula, uchoyo, umero. Kuna mtoto mdogo ambaye
alikuwa mlafi. Kaka yake alikuwa anachota karanga kwenye bakuli mtoto alikataa
kuchukua karanga na kusema kiganja chake ni kikubwa kuliko changu. Lakini na
tumbo la kaka yake lilikuwa kubwa sana.
Tusilale kwenye wivu. Kuna
barabara nyingi kwenda kwenye nyumba ya chuki. Wivu ni barabara fupi. Kuna mkristu mmoja alikuwa
mcha Mungu. Alisali kila mara. Maajenti wa shetani walimtafuta kumwangusha
awakuweza. Mkuu wa meshetani akamwendea akamnongonezea sikioni kaka yako
ameteuliwa kugombea ubunge.Mara huyo mkristu akakunja uso kwa hasira. Macho
yakatoka pima. Shetani akawaambia wanafunzi wake. Wivu ni siraha yetu kubwa.
Lakini tunazosiraha za kupambana na siraha za shetani siraha za mwanga. Wivu ni kama kupiga risasi likakurudia.
Mtu mmoja mtengenezaji wa beseni alimwonea wivu mwenzake ambaye alikuwa anaosha
magari na wanyama wadogo. Akamwambia mfalme tembo wako mweusi anaweza kuoshwa
akawa mweupe na yule jamaa mwoshaji ni mtaalamu sana. Alitaka kumwaharibia
muda wake. Yule mwoshaji alipoitwa alisema naweza ila naomba huyo mtengenezaji
beseni anitengenezee beseni ambapo tembo ataingia mzima. Yule mwoshaji
akatengeneza beseni lakini tembo akavunja beseni zote zilizotengenezwa.
Mwishoni mwenye wivu alihumia yeye.
Tusilale
kwenye mapigano. Siku ya
Ijumaa Kuu huwa tunasoma maneno haya, “Ili litimizwe lile neno alilolisema,wale ulionipa
sikumpoteza hata mmoja wao. Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta,
akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lakeni Malko. Basi
Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa
Baba, mimi nisikinywee"
Hivyo katika
kipindi hiki cha majilio tunaalikwa sote kuangalia tumeanguka wapi( mapungufu
yetu) na kuomba msamaha kwa Mungu kwa yale yote tutakayokuwa tumemkosea yeye na
pia kuwaomba msamaha wale ambao tumewakosea iwe kwa bahati mbaya au kwa
makusudi. Katika kipindi hiki tunaitwa wote kuvaa sura ya Yesu ( tobe Christ
like) ili wale tutakao wahubiria na kukutana nao waone kweli tumevaa sura ya
Yesu kufuatana na maneno na matendo yetu.
0 Response to "MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 1 YA MAJILIO MWAKA A WA KANISA."
Chapisha Maoni