OKTAVA NA HISTORIA YAKE
Octava, yaani siku nane kuanzia jumapili ya ufufuko
wa Bwana wetu Yesu Kristu hadi Jumapili ya pili ya Pasaka ( Jumapili ya huruma
ya Mungu) twaweza ona kuwa huu utamaduni katika Kanisa una mizizi na historia
yake:
Utamaduni wa hizi siku
nane kuadhimishwa ibada kwa heshima ya sherehe fulani katika Kanisa historia
yake twaweza ipata kama ifuatavyo.
Kwanza kabisa huu
utamaduni ulianzishwa chini ya mfalme Constatine wakati ambapo sherehe za
kutabaruku makanisa makubwa ya Yerusalemu, Tyre, na Lebanoni zilifanywa ndani
ya siku nane. Baada ya hapo mfumo huo wa kufanyika siku nane baada ya sherehe
uliingizwa pia katika sikukuu za Pasaka,
Pentekoste, na Epifania. Hivyo ni kwa msingi huo tunaona mwazo wa siku nane za
kusali kwa ajili ya heshima ya siku iliyotangulia kufuatana na uzito wake. Hii
ilikuwa ikifanyika mnamo karne ya nne. Na kama tufahamuvyo kuwa Pasaka huwa ni
kipindi ambapo watoto na wakatekumeni wanabatizwa, basi katika kipindi hiki cha
siku nane baada ya ufufuko wa Bwana kilikuwa pia kipindi kwa wale waliobatizwa
na kupokelewa Kanisani kama muda wao wa furaha na kutafakari.
Kadiri ya historia,ni
kwamba kulikuja maendeleo zaidi juu ya huu utamaduni wa octava za hizi sikukuu
nilizozitaja hapo juu. Kuanzia karne ya 4 hadi karne ya 7, wakristu waliendelea
na huo utaratibu wa kusheherekea hizo siku nane japo katikati ya hizo siku
kungelitokea ibada nyingine ambazo zingelisheherekewa. Krismasi ilikuwa pia
sikukuu nyingine ambayo nayo iliingizwa katika sherehe ambazo zilitengwa kuwa
na Oktava. Hadi kufikia mnamo karne ya 8, Roma tayari ilishaanzisha mfumo wa
octava siyo tu kwa Pasaka, bali hata kwa Pentekoste, Krismasi,Epifania na pia
sikukuu ya Kutabarukiwa kwa Makanisa Makuu huko Roma.
Pia kuanzia Karnne ya
saba pia sikukuu za watakatifu nazo zilianza kuwa na siku za octava, yaani siku
ya nane ya sherehe ya mtakatifu fulani, mfano kwa hilo ambapo octava zilifanyika
kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaheshimu watakatifu ilikuwa kwenye sikukuu za
watakatifu Peter, Paul, Lawrence na mtakatifu, Agnes. Kuanzia Karne ya 12 huu
utaratibu wa octava ulianza kujikita zaidi kuanzia siku ya kwanza ya oktava
hadi siku ya nane, na siku ya nane ikiwa inajumuishwa katika hayo maadhimisho.
Kuanzia zama za kati, okatava kwa ajili ya sikukuu mbalimbali zilikuwa
zinaadhimishwa kufuatana na utaratibu wa Jimbo au kufuatana na utaratibu wa
shirika la kitawa na mipangilio yake kwa ujumla.
HISTORIA YA SASA NA UTARATIBU WA OKTAVA.
1. Kuanzia Papa Pio V-
Papa Pio XII
Chini ya uongozi wa
Papa Pio V octava zilipata kuwekwa kwenye makundi mbalimbali. Pasaka na
Pentekoste okatava zake zilipewa umuhimu wake na umaalumu wake, hapa tunaona
kwamba
katika kipindi hicho
hakuna sherehe yoyote ambayo kama ingelitokea kuangukia katika octava za
sikukuu hizo ingelisheherekewa kutokana na uzito wa hizo siku zilizotajwa hapo
juu. Krismas na, Epifania na sherehe ya mwili na damu ya Yesu pia hivyo
vilipewa nafasi maalumu ambapo kama ingelitokea sikukuu ambayo ina umuhimu wake
ingelisheherekewa ndani siku za oktava za hizo sikukuu zilizotajwa.
Kuepuka kujirudia rudia
kwa maadhimisho ya namna hiyo, Papa Leo XIII na Papa Pio X waliweza kufanya
marekebisho fulani katika mchakato mzima wa hayo maadhimisho, ambapo waliweza
kuchambua octava ambazo zilipewa uzito mkubwa na umuhimu sana katika
makundi matutu ambayo kimsingi ni 1.
Oktava zilizopewa nafasi ya pekee na uzito wa pekee, 2. Oktava za kawaida, na
3. Oktava ndogo
Katika Oktava ambazo
zilipewa umuhimu na uzito wa juu, yaani Oktava za kundi la kwanza pia tunaona
kuwa nazo hizo zilipangwa kimadaraja, yaani daraja la kwanza, la pili na daraja
la tatu. Mnamo katikati ya Karne ya 20, okatava zilipangwa katika mfumo na
muundo ufuatao, ambapo chini ya huu mfumo au muundo sheherehe nyingine ambazo
zingeliangukia katika hizo oktava za sikukuu husika kwa namna moja au nyingine
zingeliathiriwa kwa kutosheherekewa
1.Okatava zilizopewa
umuhimu na uzito
·
Oktava zenye umuhimu sana daraja la
kwanza
o
Oktava ya Pasaka
o
Oktava ya Pentekoste
·
Oktava zenye umuhimu sana daraja la pili
o
Oktava ya Epifania
o
Oktava ya mwili na Damu ya Yesu
·
Oktava zenye umuhimu sana daraja la tatu
o
Oktava ya Krismas
o
Oktava ya Kupaa kwa Bwana
o
Oktava ya moyo mtakatifu wa Yesu.
2. Oktava za kawaida.
·
Oktava ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi
ya asili
·
Oktava ya Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu
·
Oktava ya Kuzaliwa kwa Yohane mbatizaji
·
Oktava ya sikukuu za watakatifu Peter na
Paul
·
Oktava ya kupalizwa mbinguni kwa Bikira
Maria
·
Oktava ya sikukuu ya watakatifu wote.
3. Oktava ndogo
·
Oktava ya Mtakatifu Stefano
·
Oktava ya Mtakatifu Yohane mtume
·
Oktava ya watoto mashahidi
·
Oktava ya mtakatifu Laurenti
·
Oktava ya kuzaliwa kwa Bikira Maria
Katika kuongezea hapo
ni kwamba watakatifu wasimamizi wa mataifa fulani, Jimbo, au Kanisa hao
waliadhimisha Oktava, ambapo kila siku misa na masifu ya siku yalirudiwa hadi
ile siku ya nane, isipokuwa kama hapo katikati ya hizo siku ingeliingilia siku
nyingine ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa.
Japokuwa sikukuu za
mtakatifu Laurent na kuzaliwa kwa Bikira Maria zilikuwa bado katika daraja la Oktava
ndogo, mnamo karne ya 20, zilifanywa kuwa nazo ni sherehe zilizo katika kundi
la sherehe kubwa hivyo ziliongezewa katika Kalenda ya Kilturjia. Oktava ya
Mtakatifu Laurent bado ilikuwa ikihadhimishwa wakati wa misa ya Mtakatifu
Yasinter. Oktava ya kuzaliwa kwa Bikira Maria kiasi iliwekewa kikwazo, lakini
jina takatifu na tukufu la Maria sherehe yake ilifanyika katika Oktava ya
Mateso saba ya Bikira Maria ilisheherekewa.
KUPUNGUZWA
KWA OKTAVA NA PAPA PIO XII NA PAPA PAUL
VI
Papa Pio XII aliweza
kufanya mabadiliko katika Kalenda kwa tamko alilolitoa mnamo 23 March 1955
ambapo tunaona katika hili kwamba Oktava za Krisamas, Pasaka, na Pentekoste
ndoo zilizobakia, na hivyo liturjia ya siku za Oktava ilibadilika pia, kwa
maana liturjia ilikuwa siyo ile ile, kwani kila siku ya Oktava ilikuwa na
liturjia yake. Hivyo Oktava nyingine katika Rite ya Kirumi hazikuwa na nafasi
tena. Mnamo mwaka 1969 Kanisa Katoliki lilifanya mabadiliko tena katika Kalenda
ya Kirumi kwa kuondoa Oktava ya Pentekoste.
Hivyo siku nane za
kipindi cha pasaka hutengeneza Oktava ya Pasaka na huwa daima zinahadhimishwa
kama sikukuu za Bwana zikiwa na masomo yake na sala zake maalumu ya kila siku
ya Oktava. Kuanzia 30 April 2000, Jumapili ya 2 ya Pasaka ambayo huwa ndo
inahitimisha pasaka kuanzia hapo imeitwa Jumapili ya Huruma ya Mungu.
Oktava ya Krismas
imepangwa ifuatavyo
·
Jumapili ndani ya oktava: Sherehe ya
Familia takatifu; ambayo huadhimishwa Ijumaa tarehe 30 December ikiwa Krismas
ilikuwa ni jumapili
·
26 th December: Sikukuu ya Mtakatifu
Stefano shahidi
·
27th December: Sikukuu ya Mtakatifu
Yohane Mtume
·
28th December: Sikukuu ya Watoto
mashahidi.
·
29-31 December: Sikukuu zinazoangukia
ndani ya Oktava ya Pasaka, ambapo kila siku kati ya hizo siku huwa na masomo
yake na sala zake ambapo ndani ya hizo siku, kumbukumbu za hiari zinaruhusiwa
kusheherekewa kadiri ya maelekezo ya rubrics.
·
1January ni Oktava ya Krismasi, Sikukuu
ya Bikira Maria Mama wa Mungu.
0 Response to "OKTAVA NA HISTORIA YAKE "
Chapisha Maoni