1 Response to "Revocatus paul: NJOONI NYIE MJIONEE YATAKAYOKUWA YANAJIRI KWENYE H..."

  1. Hapa ilikuwa sherehe za kupewa daraja takatifu la Ushemasi lililofanyika Jimboni Dodoma, sherehe kweli ilipendeza kama unavyoweza ukajionea ambapo Mhashamu Askofu Gerevaz Nyaisonga ndiye aliyetoa daraja takatifu la ushemasi kwa frt. Revocatus Paul. Sherehe pia ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, akiwemo spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhesh. Anna Makinda, ambaye pia aliandamana na viongozi waandamizi kutoka office za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Askofu mgatuka wa Jimbo katoliki la Dodoma, Mhashamu. Mathias Joseph, Isuja, Mkuu wa Shirika la Wapassionist Tanzania, Very, Rev. Aloysius Nguma, Mapadre wa passionist, mapadre wa mashirika mengine, mapadre kutoka jimbo la dodoma, na mapadre kutoka majimbo mengine nje ya Dodoma. Pia watawa wa kiume na kike walikuwepo kwenye sherehe ya kupewa daraja la ushemasi, ndugu jamaa na marafiki wa Shemasi Revocatus walihudhuria pia hafla hiyo ambayo ilikuwa imejaa nderemo, vifijo na vigelegele.

    JibuFuta