MAHUBIRI JUU YA JUMAPILI YA MATAWI MWAKA B

 

MAHUBIRI JUU YA JUMAPILI YA MATAWI MWAKA B.

Matukio ambayo tunaadhimisha leo, ndoo mwanzo wa kile tukiitacho juma kuu. Matukio ya jumapili ya matawi linaanzia bethania ambayo ni kilometre nne kuelekea kusini mashariki mwa Yerusalemu. Ni katika mahali hapo ambapo maelfu ya wayahudi walikwea Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya pasaka wanakutana naye Yesu.

Kwa kifupi hebu tuone injili zinasema nini juu ya safari ya kutoka Bethania kwenda Yerusalemu. Injili ya Mt. Luka inatumbia kuwa baadhi ya watu walitandaza mavazi yao njiani na wengine walitandaza matawi njiani ambapo Yesu angelipita. Mwinjili Matayo anasema vilevile kuwa baadhi walitandaza nguo zao na matawi njiani ambapo Yesu angelipita. Hivyo kwa hawa wainjili tunaona juu ya kutandaza nguo na Matawi. Mwinjili Luka natuhabarisha kwamba watu walitandika mavazi yao njiani. Hivyo tunaambiwa kuwa kutoka injili ya Matayo, Luka, na Mariko kuwa walitandaza matawi, ni kutoka katika injili ya Yohane tunaambiwa juu ya matawi ya mizeituni na kwenda kumlaki bwana.

Matawi ya Mizeituni yana maanisha nini? Hebu tuone historia: Kwa kipindi cha miaka 1000 kati ya Mfalme Daudi na Yesu. Taifa la Israeli lilitawaliwa na dola mbalimbali. Mnamo karne ya nane Israel ilitawaliwa na Waasiliano. Wasiria walitawala miliki ya kaskazini ya Israel.Katika karne ya sita tunaambiwa kuwa wababiloniani walivamia na kutawala waasiria.  Miliki ya Kusini ambayo ilikuwa miliki ya Yuda ilipinga vikali utawala wa wababiloni. Kwa msingi huo babiloni iliharibu Yerusalemu na hivyo maelfu ya wayahudi wakapelekwa uhamishoni babiloni, ila wapersia waliivamia na kuitawala babiloni. Hivyo wayahudi mateka waliokuwa wamepelekwa uhamishoni babiloni walipewa nafasi ya kurudi nchini mwao kama wangelitaka. Hivyo hekalu  lililoharibiwa na wababiloni linajengwa upya. Hata hivyo wayahudi walibaki chini ya utawala wa wa persia. Mnamo karne ya nne Alexander Mkuu aliivamia persia na kuitawala. Hivyo kwa sasa wayahudi wanakuwa katika utawala wa wagiriki. Baada ya kifo cha Alexander, himaya yake inagawanywa kwa wafuasi wake. Hivyo wayahudi wanatawaliwa na mataifa mawili, yaani mataifa ya misri na siria.

 

Mwisho tunaambiwa kuwa mnamo karne ya kwanza Yerusalemu inachukuliwa na Roma. Hata hivyo kulikuwa na kipindi kirefu kati ya utawala wa wagiriki na warumi ambapo wayahudi walikuwa huru na walifurahia uhuru wao. Waselusian chini ya mtawala antiochus epifanes walijaribu kwa nguvu zao zote kupenyeza namna yao ya maisha, zikiwemo tamaduni zao, na mila kwa wayahudi, lakini wayahudi walipinga vikali chini ya utawala wa makabayo. Neno makabayo maana yake ni Nyundo hivyo makabayo aliwapinga na kuwapiga vikali maadui wa wayahudi kati ya mwaka 163-164. Hivyo Juda makabayo aliwafukuza wagiriki wote waliokuwa wamekalia mji wa Yerusalemu. Hekalu la Yerusalemu lililokuwa limeharibiwa liliwekwa wakfu tena mnamo mwaka 164.KB. Tukio hili bado hata sasa linasheherekewa na wayahudi, sherehe ya hanuka. Wakati wagiriki wanataka kulipa kisasi cha kufukuzwa Yerusalem, lakini wayahudi wakiongozwa na Simon kaka yake na Makabayo, walifanikiwa kuurudisha mji wa Yerusalemu mikononi mwao. Hivyo kipindi cha utawala wa amani na haki kilishamiri chini ya utawala wa Simoni.

Kutoka kitabu cha kwanza cha wamakabayo wayahudi walichukua mji wa Yerusalemu kama ngome yao. Hivyo waliingia mjini humo wakiwa na matawi ya mizeituni, kwa shangwe na vigelegele huku wakiga baragumu, kwa kuwa adui mkubwa alikuwa ameshindwa na ameondolewa Yerusalemu.

Hivyo matumizi ya matawi ya mizeituni ni ishara ya ushindi mkubwa. Matawi ya Mizeituni yalitumika pia kama alama ya uhuru kwa waisraeli. Hivyo picha ya matawi ya mizeituni yalionekana pia katika fedha ya wayahudi tokea mwaka 140-70 baada ya Kristu. Lakini kabla ya hapo wayahudi chini ya utawala wa warumi walikuwa na kiu ya kumpaka mpakwa mafuta aidha kutoka katika familia ya makabayo/ Daudi ambaye angeliangamiza dola ya warumi, na hivyo kuiondoa Yerusalemu chini ya utawala wa watu wa mataifa. Hivyo umati unamkaribisha Yesu kwa matawi, ishara ya utaifa wa makabayo, mtu ambaye alikuwa anasubiriwa akiwa kielelezo cha Makabayo, Simoni au Daudi. Hivyo huyo alitegemewa kuwa mmoja ambaye angelitupilia mbali utawala wa warumi.

 

Hivyo hayo ndoo alikumbana nayo Yesu. Kumbuka alivyowalisha maelfu vipande vitano vya mikate na samaki wawili kwa fikra zao walijua kuwa ni mwenye uwezo mkubwa hivy0 walitaka kumfanya mfalme ili awaondoe katika utawala wa warumi. Kadiri ya injili ya Mtakatifu Yohane, Yesu baada ya kuona hivyo aliondoka na kwenda katika milima ya mizeituni kuomba na kusali. Kitu cha namna hiyo kinatokea pia katika jumapili ya matawi, ambapo watu wanamshangilia Yesu na kumwita Hosana mwana wa Daudi, mbalikiwa ni yeye ajaye kwa jina la Bwana  Mfalme wa wayahudi.

 

Yesu kwa kujua kilicho akilini mwao, anaingia Yerusalemu siyo kwa farasi au gari la kukokotwa na farasi, bali anaingia mjini humo kwa punda. Hilo ni jibu lake kwao lenye ujumbe mkubwa japo haongei ila tendo ambalo analifanya ni jibu tosha kwao. Hivyo huyo siye mfalme ambaye alikaribishwa kwa matawi ya mizeituni. Yesu anawaweka watu huru, siyo kwa namna ya makabayo na wenzake. Ushindi wa Yesu unaenda mbele zaidi ya ule wa makabayo. Ushindi wa Yesu siyo ule ushindi wa mtizamo wa kivita. Ijumaa kuu tutaona Yesu amenyanyuliwa Juu ya Msalaba, kunyanyuliwa kwake Juu ya msalaba ndoo ushindi mkubwa ambao utatuweka huru kutoka nguvu za dhambi na mauti.

Related Posts:

0 Response to "MAHUBIRI JUU YA JUMAPILI YA MATAWI MWAKA B"

Chapisha Maoni