OKTAVA NA HISTORIA YAKE

                   OKTAVA NA HISTORIA YAKE

Octava, yaani siku nane kuanzia jumapili ya ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu hadi Jumapili ya pili ya Pasaka ( Jumapili ya huruma ya Mungu) twaweza ona kuwa huu utamaduni katika Kanisa una mizizi na historia yake:
Utamaduni wa hizi siku nane kuadhimishwa ibada kwa heshima ya sherehe fulani katika Kanisa historia yake twaweza ipata kama ifuatavyo.

Kwanza kabisa huu utamaduni ulianzishwa chini ya mfalme Constatine wakati ambapo sherehe za kutabaruku makanisa makubwa ya Yerusalemu, Tyre, na Lebanoni zilifanywa ndani ya siku nane. Baada ya hapo mfumo huo wa kufanyika siku nane baada ya sherehe uliingizwa pia katika  sikukuu za Pasaka, Pentekoste, na Epifania. Hivyo ni kwa msingi huo tunaona mwazo wa siku nane za kusali kwa ajili ya heshima ya siku iliyotangulia kufuatana na uzito wake. Hii ilikuwa ikifanyika mnamo karne ya nne. Na kama tufahamuvyo kuwa Pasaka huwa ni kipindi ambapo watoto na wakatekumeni wanabatizwa, basi katika kipindi hiki cha siku nane baada ya ufufuko wa Bwana kilikuwa pia kipindi kwa wale waliobatizwa na kupokelewa Kanisani kama muda wao wa furaha na kutafakari.

Kadiri ya historia,ni kwamba kulikuja maendeleo zaidi juu ya huu utamaduni wa octava za hizi sikukuu nilizozitaja hapo juu. Kuanzia karne ya 4 hadi karne ya 7, wakristu waliendelea na huo utaratibu wa kusheherekea hizo siku nane japo katikati ya hizo siku kungelitokea ibada nyingine ambazo zingelisheherekewa. Krismasi ilikuwa pia sikukuu nyingine ambayo nayo iliingizwa katika sherehe ambazo zilitengwa kuwa na Oktava. Hadi kufikia mnamo karne ya 8, Roma tayari ilishaanzisha mfumo wa octava siyo tu kwa Pasaka, bali hata kwa Pentekoste, Krismasi,Epifania na pia sikukuu ya Kutabarukiwa kwa Makanisa Makuu huko Roma.


Pia kuanzia Karnne ya saba pia sikukuu za watakatifu nazo zilianza kuwa na siku za octava, yaani siku ya nane ya sherehe ya mtakatifu fulani, mfano kwa hilo ambapo octava zilifanyika kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaheshimu watakatifu ilikuwa kwenye sikukuu za watakatifu Peter, Paul, Lawrence na mtakatifu, Agnes. Kuanzia Karne ya 12 huu utaratibu wa octava ulianza kujikita zaidi kuanzia siku ya kwanza ya oktava hadi siku ya nane, na siku ya nane ikiwa inajumuishwa katika hayo maadhimisho. Kuanzia zama za kati, okatava kwa ajili ya sikukuu mbalimbali zilikuwa zinaadhimishwa kufuatana na utaratibu wa Jimbo au kufuatana na utaratibu wa shirika la kitawa na mipangilio yake kwa ujumla.


HISTORIA YA SASA  NA UTARATIBU WA OKTAVA.

1. Kuanzia Papa Pio V- Papa Pio XII
Chini ya uongozi wa Papa Pio V octava zilipata kuwekwa kwenye makundi mbalimbali. Pasaka na Pentekoste okatava zake zilipewa umuhimu wake na umaalumu wake, hapa tunaona kwamba
katika kipindi hicho hakuna sherehe yoyote ambayo kama ingelitokea kuangukia katika octava za sikukuu hizo ingelisheherekewa kutokana na uzito wa hizo siku zilizotajwa hapo juu. Krismas na, Epifania na sherehe ya mwili na damu ya Yesu pia hivyo vilipewa nafasi maalumu ambapo kama ingelitokea sikukuu ambayo ina umuhimu wake ingelisheherekewa ndani siku za oktava za hizo sikukuu zilizotajwa.


Kuepuka kujirudia rudia kwa maadhimisho ya namna hiyo, Papa Leo XIII na Papa Pio X waliweza kufanya marekebisho fulani katika mchakato mzima wa hayo maadhimisho, ambapo waliweza kuchambua octava ambazo zilipewa uzito mkubwa na umuhimu sana katika makundi  matutu ambayo kimsingi ni 1. Oktava zilizopewa nafasi ya pekee na uzito wa pekee, 2. Oktava za kawaida, na 3. Oktava ndogo


Katika Oktava ambazo zilipewa umuhimu na uzito wa juu, yaani Oktava za kundi la kwanza pia tunaona kuwa nazo hizo zilipangwa kimadaraja, yaani daraja la kwanza, la pili na daraja la tatu. Mnamo katikati ya Karne ya 20, okatava zilipangwa katika mfumo na muundo ufuatao, ambapo chini ya huu mfumo au muundo sheherehe nyingine ambazo zingeliangukia katika hizo oktava za sikukuu husika kwa namna moja au nyingine zingeliathiriwa kwa kutosheherekewa


1.Okatava zilizopewa umuhimu na uzito
·         Oktava zenye umuhimu sana daraja la kwanza
o   Oktava ya Pasaka
o   Oktava ya Pentekoste
·         Oktava zenye umuhimu sana daraja la pili
o   Oktava ya Epifania
o   Oktava ya mwili na Damu ya Yesu
·         Oktava zenye umuhimu sana daraja la tatu

o   Oktava ya Krismas
o   Oktava ya Kupaa kwa Bwana
o   Oktava ya moyo mtakatifu wa Yesu.

2. Oktava za kawaida.
·         Oktava ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili
·         Oktava ya Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu
·         Oktava ya Kuzaliwa kwa Yohane mbatizaji
·         Oktava ya sikukuu za watakatifu Peter na Paul
·         Oktava ya kupalizwa mbinguni kwa Bikira Maria
·         Oktava ya sikukuu ya watakatifu wote.


3. Oktava ndogo
·         Oktava ya Mtakatifu Stefano
·         Oktava ya Mtakatifu Yohane mtume
·         Oktava ya watoto mashahidi
·         Oktava ya mtakatifu Laurenti
·         Oktava ya kuzaliwa kwa Bikira Maria

Katika kuongezea hapo ni kwamba watakatifu wasimamizi wa mataifa fulani, Jimbo, au Kanisa hao waliadhimisha Oktava, ambapo kila siku misa na masifu ya siku yalirudiwa hadi ile siku ya nane, isipokuwa kama hapo katikati ya hizo siku ingeliingilia siku nyingine ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa.

Japokuwa sikukuu za mtakatifu Laurent na kuzaliwa kwa Bikira Maria zilikuwa bado katika daraja la Oktava ndogo, mnamo karne ya 20, zilifanywa kuwa nazo ni sherehe zilizo katika kundi la sherehe kubwa hivyo ziliongezewa katika Kalenda ya Kilturjia. Oktava ya Mtakatifu Laurent bado ilikuwa ikihadhimishwa wakati wa misa ya Mtakatifu Yasinter. Oktava ya kuzaliwa kwa Bikira Maria kiasi iliwekewa kikwazo, lakini jina takatifu na tukufu la Maria sherehe yake ilifanyika katika Oktava ya Mateso saba ya Bikira Maria ilisheherekewa.


KUPUNGUZWA KWA OKTAVA NA  PAPA PIO XII NA PAPA PAUL VI

Papa Pio XII aliweza kufanya mabadiliko katika Kalenda kwa tamko alilolitoa mnamo 23 March 1955 ambapo tunaona katika hili kwamba Oktava za Krisamas, Pasaka, na Pentekoste ndoo zilizobakia, na hivyo liturjia ya siku za Oktava ilibadilika pia, kwa maana liturjia ilikuwa siyo ile ile, kwani kila siku ya Oktava ilikuwa na liturjia yake. Hivyo Oktava nyingine katika Rite ya Kirumi hazikuwa na nafasi tena. Mnamo mwaka 1969 Kanisa Katoliki lilifanya mabadiliko tena katika Kalenda ya Kirumi kwa kuondoa Oktava ya Pentekoste.

Hivyo siku nane za kipindi cha pasaka hutengeneza Oktava ya Pasaka na huwa daima zinahadhimishwa kama sikukuu za Bwana zikiwa na masomo yake na sala zake maalumu ya kila siku ya Oktava. Kuanzia 30 April 2000, Jumapili ya 2 ya Pasaka ambayo huwa ndo inahitimisha pasaka kuanzia hapo imeitwa Jumapili ya Huruma ya Mungu.Oktava ya Krismas imepangwa ifuatavyo
·         Jumapili ndani ya oktava: Sherehe ya Familia takatifu; ambayo huadhimishwa Ijumaa tarehe 30 December ikiwa Krismas ilikuwa ni jumapili
·         26 th December: Sikukuu ya Mtakatifu Stefano shahidi
·         27th December: Sikukuu ya Mtakatifu Yohane Mtume
·         28th December: Sikukuu ya Watoto mashahidi.
·         29-31 December: Sikukuu zinazoangukia ndani ya Oktava ya Pasaka, ambapo kila siku kati ya hizo siku huwa na masomo yake na sala zake ambapo ndani ya hizo siku, kumbukumbu za hiari zinaruhusiwa kusheherekewa kadiri ya maelekezo ya rubrics.

·         1January ni Oktava ya Krismasi, Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu.

Related Posts:

0 Response to "OKTAVA NA HISTORIA YAKE "

Chapisha Maoni