MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 1 YA MAJILIO MWAKA A WA KANISA.

MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 1 YA MAJILIO MWAKA  A

MASOMO
1.Isa.2:1-5
2.Rum.13:11-14
3.Mt. 24: 37-44

TAFAKARI: TUNAALIKWA  KUJIWEKA TAYARI MDA WOTE ILI KUMPOKEA KRISTO MASIHA MAISHANI MWETU DAIMA
Katika Masomo ya leo, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kipindi kizima cha mwaka C wa Kanisa ambao umemalizika na tumeanza kipindi kingine cha Mwaka wa Kanisa, yaani mwaka A wa Kanisa ambao huanza kwa kipindi cha Majilio( Advent) kama miaka yote tufanyavyo. Kipindi hiki cha Advent, ambacho asili ya neno Advent linatokana na neno la Kilatini, yaani Adventus, maana yake kuja au “ ujio” Wakati wa Kipindi cha Majilio kabla ya kuwepo Pasaka, kipindi hiki kilikuwa kinajulikana kama kipindi cha kufunga( fasting) na kujinyima( abstinence) kwa ajili ya wahitaji na ndiyo maana Padre au watumishi wa altare huvaa mavazi ya rangi ya zambarau kama vile kwenye kipindi cha Kwaresma.
Kwa mantiki hii ni kwamba kipindi hiki cha majilio kinatualika kujiandaa kwa ujio wa Mwokozi wetu Yesu Kristu. Lakini yatupasa tujiulize kuwa ujio huu maana yake nini?
Kwa kutafakari juu ya hilo tunaweza kuelezea juu ya ujio wa Yesu Kristu kuwa ni wa aina tatu. Ya kwanza ni kuzaliwa kwake, yaani umwilisho wake uliotabiriwa na manabii( Incarnation), nafsi ya pili ya utatu mtakatifu, ya pili ni ni ujio wa Kristu ambao huwa tunausibiri hata ukamilifu wa dahali. Katika kanuni ya imani yetu hili limejielezea. Katika ule ujio watatu wa Yesu Kristu ni pale tunapomsubilia yesu mfufuka ambaye yupo miongoni mwetu, huu ujio wa tatu hauongelei Yesu aliyekufa na kuhaidi kuja au yesu atakaye kuja ( The await for Jesus coming is not ascribed only in past or future, but it is also already in the present). Ujio huo wa tatu wa Kristu kati yetu tunauona na tunaupata kupitia huduma za kanisa kama vile Sakramenti na Neno la Mungu, hivyo  ujio wa Kristu daima unakuwa kati yetu na siyo hadi kipindi cha majilio.
Kutokana na Mwanadamu kutokuwa mkamilifu, na kuanguka dhambini Mungu aliweka sheria kupitia Sheria na Manabii kuweza kumkumbusha mwanadamu wajibu wake lakini hilo halikutosha, hivyo Mungu aliamua kumtuma mwanae wa pekee kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu nah ii inadhihirishwa na Mtakatifu paul anaposema “ wakati ulipotimia Mungu alimtuma mwanae duniani (Gal4:4)
Kuja Kwa Kristo Yesu duniani na kujimwilisha kwake kulilenga  kutangaza habari njema kwa watu wote wa kila lika kama nabii isaya asemavyo “ Roho wa Bwana yu juu yangu, amenipaka mafuta,  amenituma kutangaza habari njema kwa maskini, wafungwa, kufungua vipofu, na kwa walioonewa  Na kutangaza mwaka wa Bwana.”( Cf.Lk4:18-19). Ujio wa Kristu kwa mara ya pili unatualika sote tuwe tayari kwa kuwa hatujui siku wala saa.
Kristu kwa kuja kufanya vipofu waone, alikuja kuleta mwanga ambao ungelifungua macho na moyo wa kila mmoja wetu, kuja kwake Kristu kwa maisha yetu kumefungua vipi mioyo yetu kwa sasa na mazingira yetu tunayoishi hasa mazingira ya  ushirikina, uchawi, utandawazi, technolojia, (japo hatuhalalishi kuwa teknolojia ni mbaya ila matumizi yake mabaya kupita kiasi ndiyo tatizo) ni wangapi wamefungwa macho yao na haya mambo kiasi cha kumsahau Mungu, je sisi tuliofunguliwa macho tunawafungua pia ambao bado hawajafunguliwa macho?  Katika somo la Pili, Rum. 13:1-14 Mtakatifu Paul anatwambia juu ya kuvaa silaha za nuru, akimaanisha kuwa sisi ni wana wabatizwa katika Kristu, hivyo inatupasa tuweke mioyo yetu tayari kwa ajili ya Kristu. Kuna Mhubiri mmoja maarufu alisema haya “Tujitwalie siraha za mwanga. Biblia ni siraha ya mwanga. Sala ni siraha ya mwanga. Jambo la msingi ni kutumia siraha hizo. Breki kama hauzitumii utajikuta kwenye kichaka, kwenye mtaro wa barabara.Tusilale kwenye ulafi. Ulafi ni uroho. Upapiaji chakula, uchoyo, umero. Kuna mtoto mdogo ambaye alikuwa mlafi. Kaka yake alikuwa anachota karanga kwenye bakuli mtoto alikataa kuchukua karanga na kusema kiganja chake ni kikubwa kuliko changu. Lakini na tumbo la kaka yake lilikuwa kubwa sana.Tusilale kwenye wivu. Kuna barabara nyingi kwenda kwenye nyumba ya chuki. Wivu ni barabara fupi. Kuna mkristu mmoja alikuwa mcha Mungu. Alisali kila mara. Maajenti wa shetani walimtafuta kumwangusha awakuweza. Mkuu wa meshetani akamwendea akamnongonezea sikioni kaka yako ameteuliwa kugombea ubunge.Mara huyo mkristu akakunja uso kwa hasira. Macho yakatoka pima. Shetani akawaambia wanafunzi wake. Wivu ni siraha yetu kubwa. Lakini tunazosiraha za kupambana na siraha za shetani siraha za mwanga. Wivu ni kama kupiga risasi likakurudia. Mtu mmoja mtengenezaji wa beseni alimwonea wivu mwenzake ambaye alikuwa anaosha magari na wanyama wadogo. Akamwambia mfalme tembo wako mweusi anaweza kuoshwa akawa mweupe na yule jamaa mwoshaji ni mtaalamu sana. Alitaka kumwaharibia muda wake. Yule mwoshaji alipoitwa alisema naweza ila naomba huyo mtengenezaji beseni anitengenezee beseni ambapo tembo ataingia mzima. Yule mwoshaji akatengeneza beseni lakini tembo akavunja beseni zote zilizotengenezwa. Mwishoni mwenye wivu alihumia yeye.


Tusilale kwenye mapigano. Siku ya Ijumaa Kuu huwa tunasoma maneno haya, “Ili litimizwe lile neno alilolisema,wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao. Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lakeni Malko. Basi Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee"

Hivyo katika kipindi hiki cha majilio tunaalikwa sote kuangalia tumeanguka wapi( mapungufu yetu) na kuomba msamaha kwa Mungu kwa yale yote tutakayokuwa tumemkosea yeye na pia kuwaomba msamaha wale ambao tumewakosea iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Katika kipindi hiki tunaitwa wote kuvaa sura ya Yesu ( tobe Christ like) ili wale tutakao wahubiria na kukutana nao waone kweli tumevaa sura ya Yesu kufuatana na maneno na matendo yetu.

Related Posts:

0 Response to "MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 1 YA MAJILIO MWAKA A WA KANISA."

Chapisha Maoni