Masomo:
I.Isa.7:10-14
II.Rum.
1:1-7
III.
Mt. 1:18-25
TAFAKARI:
PALIPO NA MKONO WA MUNGU HAPAKOSI HAKI NA HURUMA.
Tunapotafakari
juu ya masomo yetu ya leo, tafakari inayotuongoza ni kuwa palipo na Mkono wa
Mungu hapakosi haki na huruma. Katika
somo la kwanza tunasikia Bwana akinena kwa mfalme Ahazi kupitia kwa nabii Isaya “Tazama , Bikira
atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye atamwita jina lake Imanuel” Leo
katika somo la injili hayo yaliyosemwa na nabii isaya yanatimia.
Katika
somo letu la injili hatuna budi hasa kuwaangalia wahusika waliotajwa , yaani
Yusufu na Maria.Tunaona wazi Yusufu alipokuwa akifikiria hayo Basi tazama
malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto akisema Basi Yusufu mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariamu Mkeo
maana amepata Mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu.(Yoh1:20) Tukitafakari zaidi
maandiko haya matakatifu, kwanza tunakutana na jina ‘Yusufu’ likiwa na maana ya
“Mungu atakuongoza”. Katika maisha yetu
sisi wakristu huyu Yusufu anakuwa kielelezo kwetu na tunajifunza yafuatayo
kutoka kwake.
Yusufu,
kadiri ya Sheria ya wakati ule ( Dt: 22:23-24) iliweka wazi na bayana kuwa kama
mwanamke Bikira angelijiusisha na zinaa kabla ya kuolewa na akapatikana na
mimba adhabu yake ilikuwa kupigwa mawe hadi kufa. Hivyo kadiri ya sheria hiyo
Yusufu alikuwa na haki ya kumhadhibu mke wake ambaye kabla hajajihusisha naye
alimkuta akiwa na mimba, kwa msingi huu Bikira Maria angelipigwa mawe hadi
kufa, na Yusufu alijua hilo, ila yeye kwa hekima yake na huruma hakufanya
hivyo, neno lilomwongoza asifanye hivyo ni kusikia sauti ya Mungu kupitia kwa
malaika, hapa tunajifunza juu ya kutokuwa wepesi kuanika mabaya na mapungufu ya
wenzetu ambao tunao katika jamii, kwani kila mmoja ana mapungufu yake na hakuna
mkamilifu. Tukilitafakari jina Yusufu, yaani Mungu atakuongezea tunaona kabisa
kwamba Yusufu kukubali ujumbe wa malaika wa kuwa usiogope, na kuvumilia kwake
Yusufu ilikuwa ni mpango wa Mungu kutuletea Mkombozi, yaani Yesu Kristu.
Yusufu
anatoa somo au fundisho kuwa binadamu hayupo kwa ajili ya sheria ila sheria ipo
kwa ajili ya kumsaidia mwanadamu, na kama haiwezi pia sheria hiyo yaweza
vunjwa. Hilo linajionesha pale Yusufu alipokuwa na moyo wa Huruma na uvumilivu
kwa Bikira Maria alipokuwa na mimba ya mtoto yesu, kadiri ya sheria angelifanya
kama ilivyotaka ,na Maria angelipigwa mawe hadi kufa, lakini kinyume chake
Yusufu anahubiri huruma na msamaha, na
hili pia linajitokeza kwa Kristu mwenyewe ambaye alizaliwa naye akafanya
matendo ya huruma jinsi hiyo, tukikumbuka pale yesu alipoletewa mwanamke
aliyekamatwa kwenye uzinzi ili apigwe mawe kadiri ya sheria, kinyume chake yesu
aliwageukia na kuwaambia waliomleta ili wampige mawe, kuwa ambaye hana kosa au hajawahi kutenda kosa awe
wa kwanza kumpiga Yule mwanamke, aliposema hivyo, hata hakuna aliyethubutu
kumpiga Yule mwanamke. Hii inaonesha kuwa Kristu mwenyewe alikuwa ni
mwanamapinduzi wa sheria zilizokuwa zipo kwa ajili ya kuwakandamiza watu. Hapa tunapata fundisho nasi kuwa kabla
hatujatoa hukumu kwa wengine nasi pia yatubidi tujichunguze na tuone pia
madhaifu na mapungufu yetu.
Yusufu
anatufundisha juu ya kupigana na kuondoa roho ya woga. Kuna Mhubiri mmoja
alisema yafuatayo katika mahubiri yake:
““Siri
ya kutoogopa ni kuelewa lile linalokuogopesha,” alisema Deborah Wiles. Alipokuwa akifikiria hayo, tazama, malaika wa Bwana
alimtokea ghafla katika ndoto, akasema: “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope
kumpokea Maria kuwa mke wako, maana mimba yake ameipata kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu:” (Mathayo 1: 20). Malaika wa Bwana anaufunua utambulisho wa Yesu na
anamwezesha Yozefu kuelewa mpango wa Mungu wa wakovu.
Nakubaliana na Corrie Ten Boom
aliyesema: “Usiogope kamwe kuweka yajayo yasiyojulikana mikononi mwa Mungu
anayejulikana.” Kazi ya Roho Mtakatifu ambaye ni Mkono wa Bwana ni kuelewesha:
“Lakini atakapokuja yeye, Roho wa ukweli, atawaongoza katika ukweli wote”
(Yohane 16: 13). Askofu wa
kianglikana ilitokea akasoma insha juu ya ukoma. Alivutiwa kijifunza kuwa
dalili ya ugonjwa ni kutokuwa na hisi katika sehemu zilizoathiriwa. Baadaye
Askofu alihudhuria mhadhara na mke wake. Walikuwa wamekaa pamoja wakisikiliza
kwa makini, ghafla Askofu alisikia mguu wake wa kulia ukiwa na mwasho. Mara
moja aliinama na kujikuana, alishangazwa na kutohisi chochote. Askofu kwa hofu
alimgeukia mke wake na kumnong’onezea, ‘Mpendwa, nafikiri nimepata ukoma!
Nimejikuna mguu wangu hapakuwepo na hisi yoyote.” “Sifikiri kuwa umepata ukoma,
mpendwa,” alimhakikishia mke wake. “Mguu
ambao umeukunakuna ni wangu, sio wako.”
Mwisho
Yosefu anatupa fundisho juu ya kuwa watii na kutoa ushirikiano na Mungu. Mungu
katika mipango yake na mwito wake kwetu sisi binadamu anatuita pia nasi tutoe
ushirikiano naye. Mfano mzuri ni kama tulivyosikia jinsi Yosefu alivyotoa
ushirikiano na Mungu katika kufanikisha mpango wa Mungu wa kutuletea Masiha
ambaye tuna ngojea kuzaliwa kwake kati yetu. Yusufu hakushiriki kwa maneno hata
kwa matendo, hili linajionesha katika injili ya
mtakatifu Mt.2:13-14, 19-23. Wagiriki huwa wanamsemo usemao kuwa “
Jifunze kutii kabla ya kuamrisha” Tunavyoongelea juu ya kusikia neno, kulitenda
na kutii neno, hilo neno laweza kuwa ushauri wa wale waliotuzidi, sheria, sala,
upendo, n.k , hivyo vyote tunaalikwa tuvizingatie na tuvitende katika maisha
yetu tukiiga mfano wa Yusufu aliyesikia neno la Mungu na akatenda
0 Response to "MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 4 YA MAJILIO MWAKA A"
Chapisha Maoni