MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 32 YA MWAKA C

MAHUBIRI JUMAPILI YA 32 MWAKA C

Masomo

1.2Mak7:1-2,9-14
2.2Thes 2:16-3:1-5
3.Lk20: 27-38

Tafakari: Maisha ya hapa duniani siyo nukta,ila ni mkato wa safari ya Maisha ya Mbinguni.

Jumapili ya 32 ya mwaka tunaambiwa juu ya maisha ya baadaye. Maisha yetu hapa duniani. katika masomo yetu ya leo hili linajidhihirisha kwenye masomo yetu ya leo hasa tukianza na somo la kwanza ambalo limetoka kwenye kitabu cha Wamakabayo, Mk,7:1-2,9-14, ambapo tunaona ndugu saba wanalazimishwa kula nyama Ya nguruwe kwa shuruti, na wao wanakataa kula nyama hiyo kwa kuwa tayari hata kwa lolote ambalo lingetokea, iwe kifo au chochote, hii ilidhihirisha kwamba hawa ndugu saba waliamini juu ya ufufuko ambao ndo msingi na imani yetu sisi wakristu, kwamba mwisho wa maisha ya hapa dunia ni mwanzo wa maisha ya milele huko mbinguni. tunalojifunza kwa hawa ndugu saba ni imani kamili juu ya ufufuko. Namba saba ikiwa inamaanisha ukamilifu, hivyo ilikuwa ni kielelezo pia cha imani kamilifu ya wale wanasaba waliolazimishwa kula nyama ya nguruwe lakini hawakufanya hivyo wakiamini kuwa hata wakifa mauti bado walikuwa na tumaini kuwa maisha yanaendelea na mwisho wake siyo hapa duniani. Tunaona pia Yesu alikufa mazingira hayohayo msalabani akijua kuwa mwisho wake ni ufufuko. 
Katika injili hili linajidhihirisha pale tunaposikia Masadukayo wanajaribu kumpachangamoto Yesu Kristu juu ya ufufuko wakati wao hawakuamini juu ya ufufuko au juu ya uwepo wa Malaika, Yesu swali lao analifanyia mageuzi makubwa na kulifanya liwe fundisho kwao ambapo walileta swali hilo kama mtego na kebei ikiwepo juu yake. Masadukayo hawa kwa ujumla walikuwa kwenye tabaka la wenye hela. na hili tabaka asili yake ni kati ya wayahudi wa palestina wakiwemo kati yao, Makuhani, wamiliki wakubwa wa ardhi na wafanyabiashara matajiri ,jina sadukayo  linatokana na la Zadoki Kuhani Mkuu wa mfalme daudi 2Sam19:12 . Wao walishikilia nguvu ya mafundisho ya Torati na kuyaacha mafundisho makuu yasiyokuwa ndani ya Torati, kama vile ufufuko.
Katika hili tunaalikwa kuwa watu wa imani na matumaini kama nywele na kucha, haijalishi unazikata mara ngapi, haziachi kuota. Kuna mhubiri mmoja ambaye alisema " katika giza la tatizo uwe na matumaini" fr. Faustine Kamugisha. Mhubiri huyo anaendelea kuelezea juu ya matumaini kwamba " kama ukiwa na matumaini ya Kujenga ghorofa hewani, ni lazima uanze kujenga msingi kuanzia chini, si kwamba mambo ni magumu ndio maana hatuthubutu, ni kwasababu hatuthubutu ndiyo maana mambo ni magumu" Nasi tunaambiwa kuwa tuwe na tumaini juu ya maisha yajayo. Yesu Katika kufa kwake na kufufuka amekiwekea kifo gia ya kurudi nyuma. Ameonyesha kuwa kifo siyo nukta, bali ni alama ya mkato, sentensi ya maisha bado inaendelea.

Mafarisayo waliuliza juu ya ninani angelikuwa na halali ya kumwoa mwanamke ambaye aliolewa na ndugu saba wote wakafa na siku ya ufufuo huyo mwaname angelikuwa wa nani??? swali ambalo waliuliza bila kujua maana yake hapo Kristu anatoa somo juu ya umuhimu wa ndoa hapa duniani kwamba ndoa ipo kuendeleza uzao na kurutubisha nchi hapa duniani, na kuonyesha kuwa ndoa umuhimu wake ni kuendeleza maisha ya hapa duniani, ambapo watu huzaliwa na kufa, hivyo kama hakuna ndoa maisha ya duniani hayatakuwepo. Hivyo fundisho hilo linaendelea zaidi kwamba baada ya kifo, maisha ya Mbinguni hayaitaji ndoa kwa kuwa ni maisha ya milele ambayo hakuna atakaye kufa tena. Yesu anaendelea kuwapa changamoto Masadukayo. kuwa wao ni wajinga wa kujua maandiko matakatifu.(Mt.22:29), Yesu kuwaonyesha masadukayo kwamba walikuwa wajinga wa maandishi anatumia torati ambayo waliishikilia kuwa kielelezo chao kuwaelezea kwamba kuna ufufuko baada ya kifo hasa kutoka katika kitabu cha torati ambacho waliamini kuwa ndo kilikuwa na mafundisho sahihi ambapo alinukuu kutoka katika kitabu cha Kutoka3:6 ambapo Mungu aliongea na Musa katika Mlima Horebu, na pia katika kichaka kilichokuwa kinaungua moto ambapo Mungu mwenyewe alijitambulisha kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaac na Mungu wa Yakobo, Mungu alipoongea na Moses alisema yeye kuwa ni Mungu wa Abraham na hakusema kuwa yeye alikuwa Mungu wa Abraham, hii ikimaanisha kuwa ni Mungu wa Abrahamu aliye hai,( wakati uliopo- Present Tense), hii inamaanisha kuwa Mungu alipoongea na Moses , inamaana Abrahamu, yakobo, na Isaac walikuwa hai, kwa mantiki hiyo kunamaisha baada ya kifo kuna ufufuko .Uthibitisho wa hili ni ufufuko wake Yesu Kristu mwenyewe. Hivyo kila akiliye kuwa yesu Kristu ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba atakuwa na uzima wa milele.

Related Posts:

0 Response to "MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 32 YA MWAKA C"

Chapisha Maoni